Jumapili, 22 Septemba 2013

UBORA WA QUR'AN

Mtume Muhammad (s.a.w) amesema: "Ubora wa Qur'an juu ya maneno mengine,ni kama vile ubora wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake" Jaamiul-Akhbaar.

Na amesema pia:" Pindi mwalimu anaposema kumwambia mtoto(mwanafunzi), BISMILLAH -RAHMAN RAHIYM, na mtoto akasema; BISMILLAH-RAHMAN RAHIYM, Mwenyezi Mungu humuandikia mtoto huyo na wazazi wake na mwalimu wake kuwa huru na moto wa Jahannam" Majmaul-Bayaan Juzuu ya 1 Sahifa ya 18.

Imam Jaafar Sadiq (a.s) amesema: " Kusoma Qur'an katika Msahafu huwapunguzia wazazi wawili adhabu(za kaburini), hata kama wao ni makafiri" Al-Kaaf Juzuu ya 1 Sahifa ya 440.

Na Imam Ali bin Abi Talib(a.s) amesema: "Mwenye kusoma Qur'an katika umma huu kisha akaingia motoni, basi (mtu) huyo ni miongoni mwa wale ambao huzichukulia aya za Mwenyezi Mungu kuwa ni upuuzi" Tafsirul-Iyaash.

Hivyo basi, inampasa kila muislam kuitukuza Qur'an Tukufu,na kuisoma na kuwafundisha watoto wetu ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu duniani na akhera.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni