Alhamisi, 19 Septemba 2013

FADHILA ZA KUSOMA QUR'AN KATIKA NYUMBA ZETU NA HASARA ZA KUTOSOMA QUR'AN MAJUMBANI MWETU. 
Dini ya Kiislam inawahimiza waislam kujenga tabia ya kupenda kusoma Qur’an majumbani mwao, ili waweze kupata Baraka mbalimbali zitokanazo na usomaji wa Qur’an, na kuepuka hasara zitokanazo na kutosoma Qur’an majumbani .
Imam Ali bin Abi Talib (a.s) amesema: “Nyumba ambayo husomwa ndani yake Qur’an, na hutajwa humo Mwenyezi Mungu Mtukufu, huongezeka Baraka zake na hutembelewa na Malaika watukufu wa Mwenyezi Mungu, na mashetani huihama;na nyumba hiyo huwapa mwangaza viumbe  waliopo mbinguni kama vile nyota zinavyowapa mwangaza  waliopo ardhini.
Na hakika nyumba ambayo haisomwi humo Qur’an, wala hatajwi humo Mwenyezi Mungu Mtukufu hupungua Baraka zake,huhama humo Malaika watukufu wa Mwenyezi Mungu na mashetani hufanya makazi katika nyumba hiyo” Al-Kaaf Juzuu ya 2 Sahifa  ya 446.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni