Uislam umempa mwanamke haki ya kumiliki mali akiwa kwa mumewe au nyumbani kwao.Ni hivi karibuni jumuia mbalimbali za kiraia zimeanza kumtetea mwanamke ili apewe haki hiyo.
Qur'an Tukufu imeeleza kinagaubaga kuhusu haki hiyo.Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: "Wala msitamani vile ambavyo Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yenu(kwa vitu hivyo) kuliko wengine.Wanaume wanayo sehemu(kamili) ya vile walivyovichuma; na wanawake nao wanayo sehemu(kamili) ya vile walivyovichuma.Na mwombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu" Surat Nisaa aya ya 32.
Aya hii inaeleza wazi kuhusu haki ya mwanamke kujimilikia mwenyewe mali alioichuma maadamu ni kwa njia ya halali au pengine alipewa zawadi na ndugu zake.haki ya mwanamke kumiliki mali
Na: Abudhar Salim
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni