Ijumaa, 20 Septemba 2013

ULAZIMA WA KUFANYA KAZI KATIKA UISLAM

Uislam ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu ambao umejikita katika nyanja mbalimbali za maisha,kama vile; uchumi, siasa, utamaduni na ustawi wa jamii. Katika suala zima la kiuchumi, uislam unamtaka muislam kufanya kazi ya halali, ili kujipatia kipato kitakachomwezesha yeye kukidhi mahitaji yake muhimu ya maisha.

Amepokea Ibnu Jarir kutoka kwa Ammarah bin Khuzaimah bin Thabit, amesema: Nilimsikia Umar bin Khattab anamwambia baba yangu: "Nini kinakuzuia kupanda ardhi yako?" Baba yangu akasema: "Mimi ni mzee nitakufa kesho" Umar akamwambia: "Nakuhimiza uipande" Hakika mimi nilimuona Umar na baba yangu wakiipanda.

Na kutoka kwa Imam as-Sadiq (a.s) amesema: " Hakika mimi najituma katika haja ambayo amenitosheleza kwayo Mwenyezi Mungu, siifanyi isipokuwa ni kwasababu yakutaka Mwenyezi Mungu anione najitolea katika kutafuta halali, je husikii kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Inapomalizika swala tawanyikeni katika ardhi na tafuteni fadhila za Mwenyezi Mungu..."

Hivyo ni muhimu kwa kila muislam kuhakikisha kuwa anajituma kwa bidii, katika kufanya kazi ya halali mfano; kilimo, uvuvi, biashara n.k ili kupata mahitaji muhimu ya maisha yake na kuepuka kuleta visingizio visivyokuwa na maana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni