Jumatatu, 7 Oktoba 2013

MAMBO SITA YATAKAYOWAINGIZA WATU PEPONI

Mtume Muhammad (s.a.w) amesema,"Nidhaminieni kwa nafsi zenu mambo sita,nitawadhamini ninyi muingizwe peponi" Mambo hayo ni haya yafuatayo:

  1. Semeni ukweli mtupu muongeapo.
  2. Tekelezeni mtoapo ahadi
  3. Kuweni waaminifu mtunze amana mnapoaminiwa.
  4. Lindeni tupu zenu msifanye zinaa
  5. Inamisheni macho yenu (msichungulie nyumba za watu wala kukagua miili ya wanawake,na wanawake pia wazuie macho yao wasikague miili ya wanaume kwani zinaa huanzia machoni).
  6. Zuieni mikono yenu (yaani msiibe,msipige watu,msiandike hundi za uongo ili kuiba kwa njia ya maandishi, kwa mfano" Mradi huu umegharimu kiasi kadhaa au utagharimu kiasi kadhaa" na kumbe sivyo, msitoe wala kupokea rushwa na maasia mengine yote ya mikono kama vile kuua n.k. msifanye)"
Hivyo ndugu zangu, tujitahidi kuhakikisha tunajitahidi kwa hali na mali kutekeleza mambo hayo sita aliyoyataja Mtume wetu Mtukufu Muhammad (s.a.w),ili aweze kutudhamini hiyo Pepo Tukufu ya Mwenyezi Mungu (s.w.t), siku hiyo ya Malipo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni