fadhila za kusoma qur'anKusoma Qur'an kuna fadhila nyingi sana kwa muislam. Hivyo Mtume(S.A.W) amewahimiza waislam kusoma kila mara, ili wapate manufaa yatokanayo na usomaji huo wa Kitabu hicho Kitakatifu cha Allah Mtukufu.
Miongoni mwa fadhila za kusoma Qur'an ni hizi zifuatazo:
Mtume(S.A.W) amesema,kumwambia Salmaan al-Farsi: " Ewe Salmaan!Jilazimishe sana kusoma Qur'an,kwani kusoma Qur'an ni Kafara kwa ajili ya madhambi na kinga dhidi ya moto na humsahalishia mtu na adhabu za Allah. Na huandikiwa thawabu za mashahidi mia moja,kila mwenye kusoma aya moja na hupewa katika kila Surah anayoisoma thawabu za Manabii na Mitume na Malaika humteremshia rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na kumuombea msamaha. Hakika Muumini anaposoma Qur'an, Mwenyezi Mungu Mtukufu humtazama kwa jicho la rehema na humpa kwa kila herufi aisomayo nuru katika Sirat.
"Ewe Salmaan! Pindi Muumin anaposoma Qur'an Mwenyezi Mungu humfungulia milango ya rehema na huumba katika kila herufi inayotoka kinywani mwake Malaika anayemsabihi Mwenyezi Mungu mpaka siku ya Kiyama."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni