- Semeni ukweli mtupu muongeapo.
- Tekelezeni mtoapo ahadi
- Kuweni waaminifu mtunze amana mnapoaminiwa.
- Lindeni tupu zenu msifanye zinaa
- Inamisheni macho yenu (msichungulie nyumba za watu wala kukagua miili ya wanawake,na wanawake pia wazuie macho yao wasikague miili ya wanaume kwani zinaa huanzia machoni).
- Zuieni mikono yenu (yaani msiibe,msipige watu,msiandike hundi za uongo ili kuiba kwa njia ya maandishi, kwa mfano" Mradi huu umegharimu kiasi kadhaa au utagharimu kiasi kadhaa" na kumbe sivyo, msitoe wala kupokea rushwa na maasia mengine yote ya mikono kama vile kuua n.k. msifanye)"
NURU YENYE HEKIMA ni blog inayoelezea habari,matukio na mafundisho juu ya dini ya Kiislam ili kuwahabarisha na kuwaelimisha waislamu kuhusu dini yao, na kuwafanya waweze kuishi katika dunia hii kwa salama na amani kabla ya kwenda kwenye maisha ya milele ambayo ni maisha ya Akhera.
Jumatatu, 7 Oktoba 2013
MAMBO SITA YATAKAYOWAINGIZA WATU PEPONI
Mtume Muhammad (s.a.w) amesema,"Nidhaminieni kwa nafsi zenu mambo sita,nitawadhamini ninyi muingizwe peponi" Mambo hayo ni haya yafuatayo:
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)