Jumatano, 28 Agosti 2013

KISA CHENYE MAFUNZO

Sami alikuwa Mzee ambaye ni kipofu .Alikuwa akiishi katika kijiji cha Minga, Mkoani Singida.Siku moja wakati wa kiza kinene, alitoka katika kibanda chake kilichojengwa kwa miti na kuezekwa kwa udongo,maarufu kwa jina la " Tembe" kwa ajili ya matembezi,ilihali mkononi mwake akiwa amebeba taa ya Karabai, huku akitembea kandokando ya barabara.
Kwa upande wa pili wa barabara,kijana mmoja aitwae Suma alikuwa akija. Wakati kijana huyo alikaribia karibu alitambua kuwa, mtu aliyebeba Karabai alikuwa ni jirani yake mzee Sami, ambaye ni kipofu.
Kijana yule alimsalimia na kumwambia, "Hakika wewe mzee Sami ni mpumbavu tena huna akili, kwa nini wabeba Karabai kizani ilihali wewe ni kipofu, itakusaidia nini?"
Mzee yule akamjibu:" Sikuibeba Karabai hii kwa ajili yangu, bali nimeichukua kwa ajili ya watu kama wewe,kwani pindi watapoiona taa hii basi hawatonipomia"
Kijana yule hakuwa na la kusema bali alitahayari na kuamua kuondoka na kwenda zake.Je,kati ya wawili hawa kipofu hasa ni nani.
MAFUNZO
Kisa hiki kinatufundisha kuwa tusiwadharau watu wenye ulemavu, kwani ni binadamu kama sisi na wanaweza kufanya jambo lenye hekima na manufaa kwa jamii.Hivyo tuwaheshimu na kuwapenda.

Jumatatu, 26 Agosti 2013

UMUHIMU WA MADRASA

Mmoja wa waalimu wa dini ya kiislam akimshukuru Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, wapili kulia wakati wa ufunguzi wa Madrasa Mjini Unguja.

Alhamisi, 22 Agosti 2013